Watanzania wawili wanahojiwa na
Polisi wa Afrika Kusini baada ya kukamatwa jana na kilo 55 za dawa za kulevya.
Watu hao wawili wanatazamiwa
kufikishwa mahakamani kesho
kujibu tuhuma za kukamatwa na dawa hizo zenye
thamani ya Rand75 milioni (Sh11.7 bilioni).
Maofisa wa Kikosi Maalumu cha
Kupambana na Makosa ya Jinai na Rushwa cha Afrika Kusini (The Hawks),
kiliwakamata watu hao katika Kitongoji cha Kempton Park, Ekurhuleni, Jimbo la
Gauteng.
Msemaji wa Hawks, Paul Ramaloko
alisema jana kuwa maofisa hao walivamia nyumba waliyokuwa wanaishi Watanzania
hao na kukuta mzigo huo.
Hata hivyo, alikataa kutaja majina
ya watu hao kwa kuhofia kuharibu uchunguzi akisema bado walikuwa wanawasaka
watuhumiwa zaidi wakiwamo raia wa Afrika Kusini.
Alisema kikosi chao kimepata
mafanikio makubwa kwa kukamata dawa nyingi kiasi hicho... “Tunakaribia
kuwakamata vinara wa biashara hiyo, maana tumeelezwa kuna kundi kubwa la watu
wazito,” alisema Ramaloko. Hii inakuwa mara ya pili katika kipindi cha miezi minne
kwa Watanzania kutuhumiwa kubeba dawa hizo.
Julai mwaka huu, wasanii wawili
Agness Gerald `Masogange’ na Melissa Edward walikamatwa kwenye Uwanja wa Ndege
wa Oliver Tambo, Johannesburg wakiwa na kilo 180 za kemikali aina ya ephedrine
zenye thamani ya Sh7 bilioni.
Baada ya kukaa miezi miwili jela,
Masogange alipatikana na hatia ya kuingiza kemikali hiyo, ambayo hutumika
kutengeneza dawa za kulevya na kutozwa faini ya Rand 15,000 (Sh2.3 milioni).
Melissa aliachiwa huru baada ya
kuonekana hana hatia.
Wasafirishaji sasa watumia samaki
Katika hatua nyingine, wasafirishaji
wa dawa za kulevya inasemekana wamebuni mbinu mpya ya kutumia samaki
kusafirisha bidhaa hiyo haramu.
Akizungumza jana wakati wa
uteketezaji wa dawa za kulevya, Mkuu wa Kitengo cha Kudhibiti Dawa za Kulevya,
Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP), Godfrey Nzowa alisema wanatumia
samaki kwa kuwa wana harufu kali.
0 comments:
Post a Comment