Saturday, 16 November 2013

UMEME KUKATIKA KWA SIKU 11 MFULULIZO NCHINI,MIKOA ITAKAYOATHIRIWA NI PAMOJA NA DAR ES SALAM,PWANI,DODOMA....

Filled under:



Wateja  katika mikoa inayopata umeme kupitia kwenye grid ya taifa wanatarajia kutapa tatizo la umeme kwa siku zisizopungua 11,hii ni kutokana na upungufu wa gesi kutoka chanzo cha songosongo kilichopo wilayani Kilwa mkoa wa Lindi

Hali Hiyo Imetajwa Kutokana na Kuwepo kwa Matengenezo ya KIiufundi Kwenye  visima vya ges  unaofanywa na kampuni ya Pan Africa energy Tanzania limited(PAT)

Meneja wa uhusiano wa tanesco,Badra Mosoud alisema upungufu huo utatokea novemba 16 hadi novemba 26 mwaka huu pia alielezea mikoa itakayoathiriwa ni pamoja na dae es salam,pwani,tanga,Kilimanjaro,arusha,Dodoma,morogoro,singida,mwanza,mara,Mbeya,Iringa,tabora,shinyanga,mara na zanzibar


Masoud  amesema ges imekuwa ikiwawezesha kutoa megawati 100 katika kituo cha Ubungo1,megawati 100 katika kituo cha Ubungo 2,kituo cha Tegeta megawati 45 katika kampuni ya songas imekuwa ilitoa  megawa 182 na kuongez a kutoka an na matengenezo hayao kutakuwa na upungufu wa megawati 150 hadi200 na kwamba uzalishaji wa umeme kutumia mafuta na maji utaendelea

Masoud ametoa wito kwa wananchi kuwa wavumilivu kwa sikuhizo wakati matengenezo yanaendelea kwa lengo la kuboresha upatikanaji wa gesi  ya kutosha kwa ajili ya kuzalisha umeme wa kutosha



0 comments:

Post a Comment